Mnyarwanda aangalia kwa kuandikwa katika kitabu cha watu waliovunja rekodi Duniani nzima ‘’WORLD GUINESS RECORD’’

Dusingizimana Eric
Mwanakriketi wa Rwanda Eric Dusingizimana jana jumatano ameanza kiapo chake kinachotarajiwa kumweka katika kitabu cha watu wenye rekodi duniani kote ‘’Guiness World Record.’’

Dusingizimana alianza jaribio lake la kupiga mpira wa kriketi masaa 51 bila kuacha. Wakati wowote akafanikiwa, atakuwa mwanaspoti wa kwanza wa mchezo wa kriketi anayepiga mpira kwa muda mrefu ‘’The longest batting cricket net holder’’ ambapo atachukuwa nafasi ya Mhindi Virag Male aliyewupiga masaa 50 bila kusimama.

Akiongea na mwanahabari, kabla ya kuanza jaribio, Dusingizimana ambaye ni mwenye umri wa miaka 29 alisema kuwa yuko tayari kuvunja rikodi hiyo bila kupumzika isipokuwa dakika 5 aliyepewa kama mapumziko baada ya kila saa.

‘’Tunahitaji kujenga kesho wa kriketi nchini Rwanda, kuanzisha huduma nzuri za kriketi kama kuboresha sura ya mchezo nje ya Rwanda, Mimi sitakuacha mpaka mpira wa mwisho.’’
Dusingizimana alisema.

Dusungizimana, ni mmoja mwa wanakriketi wenye uzoefu hapa Rwanda ambaye alianza mwaka wa 2006., Baadaye alikwenda kuwuchapa katika timu ya Young Tigers, Impala Titans hadi 2014 wakati yeye akirudi katika timu ya Right Guards.

Kiijana huo aliyekuwa mchezaji wa kwanza katika timu ya taifa tangu mwaka wa 2008, aliyehudhuria mashindano ya kriketi mjini Accra/Ghana katika mwaka wa 2011

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments