Rais mpya wa Uganda ametawazwa rasmi.

Yoweri Museveni leo ametawazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Uganda kwa muhula wa tano mfululizo.Tayari Rais Museveni amekwisha tawala miaka 30. Kutawazwa kwake leo, ambako kunashuhudiwa na viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni wengine mashuhuri, kuna fuata ushindi uliojaa ubishani katika uchaguzi wa Februari 18.

13.17pm:Miongoni mwa marais wanaohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na rais wa Sudan Omar el Bashir anayeswaka na mahakama ya uhailifu wa kivita katika eneo la Darfur na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

13.13pm:Jeshi la Uhanda latoa heshima zao kwa rais Museveni hivi sasa.
13.09pm:Wimbo wa taifa unaimbwa

12.56pm:Ni wakati ambapo ndege za jeshi zinatoa heshima zao kwa rais Museveni.Ndege hizo zinaonyesha uwezo wake wa kulilinda taifa la Uganda chini ya uongozi wa rais Museveni.

12.38pm:Museveni amekabidhiwa vifaa muhimu vya madaraka ikiwemo katiba,ngao ya mamlaka,bendera na upanga ambao ni ishara ya jeshi.
Na sasa ni zamu ya jeshi la taifa hilo kumpatia heshima rais huyo.

12.15pm:Rais Museveni alikagua gwaride la jeshi baada ya kuapishwa rasmi
12.10pm:Rais Yoweri Museveni aapishwa rasmi na jaji mkuu

12.05pm:leo rasmi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili watu watokeze kwa wingi kwa sherehe hizo. Ingawaje bado kuna hali ya wasiwasi kwa vile chama cha upinzani na FDC na mgombea urais wa zamani Dk Kizza Besigye bado wanakana ushindi wa Museveni.

12.00pm:Rais Yoweri Museveni kuapishwa kuwa rais kwa muhula wa saba mfululizo nchini Uganda

Museveni kumkabidhi madaraka Museveni si jipya kwa Waganda. nani Rais ambaye alilaumu mwaka 1986, viongozi wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu sana.

Baadhi ya watumbuizaji wa hafla hiyo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments