Rwanda yafungua upelelezi kuhusu vifo vya wahispania ambao waliouawa Rwanda

Johnstone Busingye na Felix Costales Artieda , Balozi wa Hispania nchini Rwanda ambaye ana kikao kikuu mjini Nairobi/ Kenya
Serikali ya Rwanda inasema kwamba Mahakama wa Rwanda yaanza upelelezi kuhusu vifo vya watawa watatu wenye Uraia wa Hispania waliouawa nchini Rwanda mwaka wa 1997.

Wizara ya Sheria imetangaza kwamba serikali ya Hispania imeisha kupeleka kesi hiyo kwa mahakama wa Rwanda ili iweke mahakamani watu wote waliochangia vifo hivyo wakati walikuwa kufanya hatua za kirafiki.

Jaji Fernando Andreu wa Hispania aliyetolewa nyaraka za kuwakamata maafisa 40 wa jeshi la Rwanda. Akawaagiza shutuma za mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya kibinadamu na uhalifu wa kivita na ugaidi. Baadaye Karenzi alikamatwa nchini Uingereza ndipo aliyekombowa mwaka jana.

Msemaji wa mahakama wa Rwanda Faustin Nkusi aliambia Redio K-FM kwamba Rwanda yaanza upelelezi kuhusu vifo vya watawa wenye utaifa wa Hispania.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Sheria Johnstone Busingye akikubali kuwa Hispania ilituma Kesi hiyo kwa Rwanda.

Alisema ‘’Kesi dhidi ya maafisa wa Rwanda tangu 2008 imekuwa kupelekwa kwa mahakama wa Rwanda.’’

Katika Ikulu Felix Artieda Balozi wa Hispania alisema kuwa nchi yake inataka kuimarisha Diplomasia na Rwanda.

Pia alisema kuwa nyaraka za kuwakamata viongozi wakuu 40 katika serikali na kijeshi wa Rwanda tayari kufutwa baada ya mabadiliko mapya katika kanuni za sheria huko Hispania.

Busingye kupitia Twitter

Janvier KARANGWA @Makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments