Nyarugenge : Wilaya yakubali usaidizi kwa mazishi ya mke aliyeuawa

Baada ya kifo cha marehemu Mahoro Theodosie aliyeuawa katika kituo cha mabasi cha Nyabugogo, baadhi ya waliofanya kazi pamoja nae walianza kuhangaikishwa na kulalamikia jinsi marehemu huyo atakavyozikwa wakati familia yake haina uwezo na kusema kuwa mmewe anafungwa jela , siku ya Jumapili ndipo walianza kuzunguka Nyabugogo na kuomba usaidizi wa kuzika marehemu huyo.

Katika mahojiano na Makuruki.rw mwenye mamlaka ya masuala ya kijamii wilayani Nyarugenge ametangaza kuwa wilaya imeanzisha usaidizi wa kuzika marehemu huyo.

Ndayisenga Jean Marie mwenye mamlka ya masuala ya kijamii wilayani Nyarugenge ameakana habari zinazosemwa kuwa mme wa marehemu anafungiwa Iwawa kama watu walivyotangaza, ametangaza kuwa wilaya ya Nyarugenge imeanza mpango wa kusaidia kwenye mazishi ya marehemu.

Alisema "Mme wake yupo, hakufungwa kama ilivyotangazwa, lakini tunatayalisha jinsi ya kuzika marehemu, tukishirikiana na mmewe, tumetayalisha motokaa (Coaster) ya kubeba watu watakaoenda kwenye mazishi, polisi yakubali motokaa ya kubeba maiti pia familia imesaidiwa kupata vitambulisho vya mazishi".

Ndayisenga aliendelea kwa kusema kuwa baada ya mazishi watasaidia mafilia yake na kutafuta usaidizi kwani marehemu aliacha watoto wanne wadogo. Tutamsogelea atuambie usaidizi anaohitaji.

Siku ya Jumamosi tarehe 7 Mei 2016 kwenye kituo cha mabasi Nyabugogo ndipo Mahoro Theodosie alipigwa na kufariki dunia, baada ya kifo chake jeshi la polisi lilitangaza kuwa aliuawa na Ndayisenga Joseph mfanyakazi wa kampuni ya usafi inayofanyia wilayani Nyarugenge katika tarafa la Kimisagara.

Wakati tulipoandika habari hii, jeshi la polisi ilisema kuwa Ndayizeye Joseph anayeshtakiwa kuua Mahoro Theodosie anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments