Simba yaipa Yanga ubingwa

Haruna Niyonzima nohodha wa timu ya taifa AMAVUBI wa Rwanda
Timu ya soka ya Yanga imetwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Yanga wameupata ubingwa huu bila ya kuwa uwanjani baada ya watani wao wa jadi timu ya Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa timu ya Mwadui Fc.
Kwa matokeo hayo hakuna timu yoyote yenye uwezo wa kufikisha pointi 68 ambazo wanazo Yanga hadi sasa, ambao bado wanamichezo mitatu mkononi.

Simba SC ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kufikisha pointi 67 ikishinda mechi zake zote tatu zilizobaki, wakati Azam FC inaweza kumaliza na pointi 66 ikishinda michezo yake miwili iliyobaki.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments