Floyd Mayweather kurudi tena ulingoni, kuzichapa na staa wa UFC, Conor McGregor

FLOYD MAYWEATHER na staa wa UFC, Conor McGregor wapo mbioni kuingia ulingoni kuzichapa kwenye pambano kubwa na aghali zaidi la masumbwi katika historia.

Gazeti la The Sun limedai kuwa Mayweather, anatarajia kuzichapa na staa huyo jijini Las Vegas mwaka huu.

Mayweather alitangaza kustaafu ndondi akiwa ameshinda mapambano yote 49 aliyowahi kupigana. Kwenye pambano hilo Mayweather atachukua paundi milioni 100 huku McGregor atachukua paundi milioni 7.

Tangazo rasmi litatolewa wiki chache zijazo.
Chanzo kililiambia gazeti la The Sun kuwa Floyd alichukia baada ya Conor kudai anaweza kumtwanga KO ndani ya sekunde 30 tu na sasa anataka kumuonesha kazi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments