Rwanda kuharakisha kesi za Wagonjwa, wanawake wajawazito na watoto

Waziri Busingye Johnston
Katika mahojiano na wandishi wa habari Waziri wa Sheria akiwa tena mjumbe mkuu wa Serikali ya Rwanda Johnston Busingye asema kuwa katika wiki ya usaidizi wa kisheria (legal week aid) huwenda kuharakisha kesi ya wafungwa katika vipengele maluum ikiwa pamoja na wagonjwa wenye ugonjwa hayaponyeki,wanawake wajawazito na watoto pia.

Busingye amesisitiza juu ya kesi kadhaa Rwanda ilikuwa na idadi kubwa ya kesi za wahusika wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka wa 1994 asema kwamba mahakama ya ndani hakukuwezi kuisha kesi hizo kwa muda mfupi ilikuwa muhimu kuweka ngazi nyingine ili kuisha kesi hizo.

Waziri Busingye aliwapongeza INKIKO GACACA, ABUNZI, na mawakili katika kila wilaya (MAJ) asema wao walisaidia wanaraia kuhusu shughuli za sheria.
Kiongozi huo amebainisha kwamba katika wiki hii ya usaidizi katika shughuli za sheria, serikali huenda kuhamasisha mahakama ili kuisha kesi hizo za vipengele maluum kwa haraka.

Alisema ‘’tuna watu wanaohitaji kupewa haki ya kisheria kwa haraka haraka kuhusu kesi zao.’’

Odette Yankurije mjibika wa haki za kisheria ya wanaraia katika wizara ya sheria alisema kuwa waliapa kuisha angalau kesi 30 za watoto.

Wiki maalum ya usaidizi wa kisheria kwenye ngazi ya kitaifa itazinduliwa Wilayani Gisagara tarehe 09 mwezi Mei mwaka wa 2016 alafu kuendelea wailayani mbali mbali za nchi

Wizara ya Sheria inasema kuwa kesi 120 zinazotalajiwa kuchukuwa mahakamani katika wiki hii, kesi za mali ya wanusurika yarioharibiwa wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi bado hakumalizwa hadi sasa thamani 5%.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments