Barabara Kagitumba-Kayonza-Rusumo huenda kujengwa upya.

Katika mazungumzo tarehe 30, mwezi Aprili mwaka huu na wakazi wa Wilaya ya Kayonza, Rais Paul Kagame wa Rwanda aliwahakikisha kuwa barabara inayoanzia Kagitumba-Kayonza mpaka Rusumo huenda kujengwa upya.

Alisema ‘’ barabara kubwa inayetoka Kagitumba jirani na Uganda kupitia hapa kuelekea Rusumo iko katika mpango wa kujengwa upya, vifaa muhimu tayari kupangwa, tunaitengeneza kwa ajili yenu ili kuilinda na kuitumia bora.’’

Watumiaji wa barabara walilalamika tangu zamani kuwa Kagitumba-Kayonza-Rusumo ni barabara ilioharibika sana.

Mwezi uliyopita Rais Paul Kagame na Mwenzake wa Tanzania walizindua rasmi daraja la Rusumo linalotarajiwa kuongeza biashara kati ya nchi hizo mbili na kanda kwa ujumla.

Chanzo : Kigali today

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments