Huenda MALARIA kuisha mwaka 2020

Shirika la Afya Duniani –WHO- limetangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria kuangamizwa kabisa ifikapo mwaka 2020

Ripoti iliyotolewa na WHO katika Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria imesema kuwa, kuna uwezekano ugonjwa huo utakomezwa kabisa katika nchi sita za AFRIKA zinazoshambuliwa na malaria hadi kufikia mwaka 2020.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, nchi hizo ni ALGERIA, CAPE VARDE, SWAZILAND, BOSTWANA, AFRIKA KUSINI na COMORO.

AFRIKA KUSINI imetangaza suala la kupambana na malaria kuwa ni lengo la kitaifa.
Takwimu zinaonesha kuwa, eneo la chini ya Sahara barani Afrika ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya kesi za ugonjwa wa malaria unaosababishwa na mbu aina ya Anopheles.

Asilia 88 ya wagonjwa wa malaria na asilimia 90 ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo katika mwaka uliopita wa 2015 iliripotiwa katika eneo hilo.

Chanzo : TBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments