Liverpool : Mamadou Sakho asimamishwa

Uongozi wa klabu ya Liverpool leo April 23 2016 umetangaza kumsimamisha beki wake ambaye alikuwa anahusishwa kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, Liverpool imeamua kumsimamisha beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mamadou Sakho wakati ambao UEFA wanasubiriwa kukamilisha uchunguzi wao.

Sakho ambaye anachunguzwa na UEFA toka March 17 baada ya mchezo wa Europa league kati ya Man United dhidi ya Liverpool uwanjani Old Traford, amesimamishwa na Liverpool baada ya kukaa na uongozi na kujadiliana, lakini Mamadou Sakho atakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya uchunguzi wao kukamilika.

Baada ya kuchukuliwa sample na kufanyiwa vipimo Mamadou Sakho anaaminika kutumia ‘Fat Burner’ kwa ajili ya kusisimua misuli, kitu ambacho hakikubaliki michezoni.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments