Kwenye huduma za uwekezaji na biashara, RDB yaendelea kurahisisha huduma zinazohitajika zaidi na Wananchi.

1

Bodi ya maendeleo nchini Rwanda (RDB) inaendelea kurahisishia watakao kuanzisha uwekezaji na biashara kufanyia huduma zao nchini Rwanda, ikiwemo kuandikisha shughuli hizo na kutafuta vitambulisho kwa njia rahisi na muda mfupi kupitia teknolojia.

Isipokuwa biashara, RDB imeweka nguvu kurahisisha kupata huduma zipewazo kuandikisha ardhi, kuona maji na umeme hata na vitambulisho vya kujenga kwa muda mfupi.

Katika mapinduzi yaliofanywa na RDB kwa kurahisisha uwezekazi. RDB inatangaza kuwa kuandikisha shughuli zako, hupata masaa yasiozidi sita kwa bure kupitia njia ya teknolojia, kujiandikisha na kuona TVA, hivi vyote vitafanywa kwa kutumia muda mfupi ukilinganisha na hali ya zamani.

Tushabe Karimu kiongozi wa ’Doing Business’ atangaza kuwa mapinduzi haya ya kurahisisha uwekaji huambatanishwa na kurahisisha huduma zinginezo kama kuandikisha ardhi, majengo ya biashara na mali zinginezo zinaendanazo na biashara kwa kutumia technolojia ama njia ya mobile money.

Njia hii ya internet na mobile money huhamasisha watu kulipa ushuri na vinginevyo kwa kuokoa muda. Haya yanahusu watu wanaotaka vitambulisho vya ujenzi, maji na umeme licha ya kutumia siku 15 kupitia njia hizo unapoteza dakika chache kwa kujibiwa.

Kwa tatizo la usalama kwa mtu aliyetumia njia hii ya teknolojia, Karim Tushabe amesema kuwa mtu atapewa nywila. Ameongeza kuwa usalama wanchi utasaidia kwani unaaminiwa kwa pande zote na hakuna mtu anayeweza kusita ama kuwa na tatizo.

Tushabe ameeleza “Kila mtu atapewa nywila ya kipekee. Kuhusu usalama, natumaini kuwa hakuna tatizo lolote kwani mnajua kuwa usalama wa nchi upo kwani nchi yaiwezi kulinda usalama wa nje na kusahau usalama wa teknojia, nataumaini kuwa hakuna tatizo”

Kwa tatizo la watu wengi wasojua kutumia teknolojia, "Kuna watu wenye mamalaka ya kusaidia watu hao na kuwaonyesha njia ya kupitiamo". Tusabe alieleza

Katika mapinduzi haya yaliotangazwa RDB ya kurahisisha uwekaji na kupata huduma, kuna sheria ya kushitakiwa hasara kwani mtu anaweza kusaidiwa na serikali. Tushabe alitangaza kuwa wanyarwanda wengi hawakushiriki wakati wanapopata hasara katika shughuli zao.

RDB inatangaza kuwa ukarabati huu unaanza mwezi juni 2016 na kusaidia wafanyabiashara na watakao kuanzisha biashara zao kutumia muda mfupi na fedha chache kwa kurahisisha shuguli hizo.

Karim Tushabe, mkuu wa Doing Busness

Martin Ikuramutse Hubert

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments