Kanye West na Jay Z watuhumiwa kuhusu udanganyifu

Shabiki aitwaye Justin Baker-Rhett anamshtaki Kanye West, kampuni ya Jay Z, S. Carter Enterprises, na TIDAL kwa kuahidi kuwa albamu ya Kanye West, The Life of Pablo, ingepatikana kwenye mtandao wa Tidal tu.

Ahadi hiyo imevunjwa hivi karibuni kwasababu TLOP inapatikana kwenye mitandao mingine mikubwa.
February mwaka huu, Kanye alitangaza :

My album will never never never be on Apple. And it will never be for sale… You can only get it on Tidal.

Kwa mujibu wa Rhett, uongo huo ulifanyika ili kuipa kiki Tidal iliyokuwa ikipumulia mashine. Albamu hiyo iliongeza watumiaji wa mtandao huo maradufu. Kanye ni miongoni mwa wamiliki wa Tidal, pamoja na Jay Z, Beyoncé, Madonna, Rihanna, J. Cole, na Nicki Minaj.
Rhett anataka alipwe fidia.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments