FC Barcelona wamepigwa tena na Valencia

Ligi Kuu Hispania iliendelea, huku mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Valencia ndio ulikuwa wa kuvutia zaidi kwani mashabiki wengi wa Barcelona walitaka kuona timu yao ikipata ushindi baada ya kukubali kipigo tena Nou Camp baada ya kufungwa na Madrid April 2.

FC Barcelon April 17 2016 wamekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Valencia katika uwanja wao wa Nou Camp, hivyo hilo ni pigo tena baada ya siku chache tu zimepita toka waondolewe katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madrid.

Valencia walipata goli lao kwanza dakika ya 26 kupitia kwa mchezaji wa FC Barcelona Ivan Rakitic kujifunga, goli ambalo liliwafanya FC Barcelona kupata shida kusawazisha ila Valencia wakafunga tena goli la pili dakika ya 45 kupitia kwa Santi Mina ila Lionel Messi dakika ya 63 aliipatia FC Barcelona goli la kufutia machozi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments