Blogger amfungulia kesi Wizkid inayoweza kumweka jela miaka 7

Mwandishi maarufu wa blogger nchini Nigeria, Linda Ikeji amemfungulia kesi Wizkid baada ya kutupiana maneno kwenye mitandao siku chache zilizopita.

Linda Ikeji aliandika kwenye blog yake kuwa Wizkid amepewa notice kwenye nyumba aliyokuwa amepanga baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango.

Kutokana na maneno hayo Wizkid hakufurahishwa na kitendo cha mwandishi huyo kuweka wazi mambo yake na baadaye alipost picha za Linda Ikeji mitandaoni na kuandika “If I ever see you, I’ll get my 16-year old cousin to beat the shit out of you.”
Kauli hiyo ya Wizkid imemkasirisha Linda Ikeji na kuamua kumfungulia mashtaka staa huyo kwenye kituo cha polisi kilichopo Lagos.

Sheria ya makosa ya jinai ya Nigeria kifungu cha 323, inasema : “Any person who, knowing the contents thereof directly or indirectly causes any person to receive any writing threatening to kill any person is guilty of a felony, and is liable to imprisonment for 7 years.”

Chanzo : Bongo5

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments