Polisi yanasa wanaokejeli mauaji ya kimbari Rwanda

ACP Celestin Twahirwa, msemaji wa Polisi nchini Rwanda
Polisi wa Rwanda wameripoti kuwapo kesi 40 za hivi karubuni za wanaohusika na kueneza itikadi ya mauaji ya kimbari wakati wa wiki ya kuadhimisha mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi iliyomalizika jumatano iliyopita.

Msemaji wa polisi wa Rwanda, ACP Celestin Twahira, wahusika wanafanyiwa uchunguzi kuhusu tuhuma za kueneza habari mbaya zinazolenga kukanusha na kupuuza katika jamii zao.

‘’tunaendelea ili kubaini watu wengine wanaochochea siasa za chuki na wale wanapinga kuwapo kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.
Vyombo vyetu vinaendelea kuwafuatilia watu hao’’
Kilisema chanzo kimoja cha Polisi.

Kitendo chochote cha kueneza itikadi kali juu ya mauaji ya halaiki au kukana kuwapo kwake ni kosa la jinai Rwanda

Twahirwa alisema kesi hizo zinajumuisha matamshi ya watu ambao wanaonekana kulenga kuumiza hisia za waathirika wa mauaji ya halaiki aliyotokea 1994 na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kulazmika kukimbilia uhamishoni.

Amesema kuna wale ambao wamekana kufanyika mauaji ya halaiki dhidi ya watutsi.

Halikadharika kumeripotiwa kesi ya mtu kusambaza sarafu ambazo hazitumiki tena ambazo zilitumika wakati wa utawala wa Gregoire Kayibanda.
Kayibanda anatambulika kama mmoja kati ya wachochezi wakuu wa mauaji ya halaiki ya kimbari nchini Rwanda.

Halikadhalika polisi wa Rwanda wamesema wamekamata mtu katika Wilaya ya Nyarugenge ambaye alisema kukumbuka waliouawa kwa umati mwaka 1994 ni kupoteza muda.

Watu wenye itikadi ya mauaji ya halaiki wanaokana mauji ya halaiki dhidi ya watutsi hujitokeza zaidi Aprili kila mwaka wakati wa kukumbuka mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994 na Watutsi na Wahutu wenye msimamo ya wastani zadi milioni moja waliuawa katika kipindi cha siku 100.

Chanzo : Mwananchi

Janvier KARAGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments