Ligi kuu ya Rwanda : APR FC hakuweza kutetea ubingwa wake mbele ya Etincelles Fc

Wachezaji wa Etincelles kusherehekea bao baada ya kuifunga APR FC
Bingwa mtetezi wa ligu kuu ya kandanda nchini Rwanda APR FC ilipoteza mechi ya kwanza baada ya wiki ya kukumbuka dhidI ya Etincelles (timu ya Wilaya ya Rubavu, magharibi mwa Rwanda) katika uwanja wa Kigali jana siku ya ijumaa.

Kwenye dakika 18 ya mchezo Mshambuliaji wa zamani wa timu ya wannanchi Rayon sports ambao alisaini hivi karibuni katika Etincelles Bodo Ndikumana aliifunga APR FC bao inayoiwezesha( ETINCELLES FC) kuinua kwa nafasi ya 11 kutoka eneo nyekundu.

Nizar Khanfir mzaliwa wa Tunisia bado anahitaji kutumia nguvu zaidi kwa kutetea ubingwa na kuwashawishi mashabiki kwamba ni kocha mkubwa hata kama APR FC bado kuongoza orodha kwenye nafasi ya kwanza.

Matokeo ya Mechi nyingine zilizotokea jana siku ya 16 katika Rwanda Azam premier league.

Ijumaa
SC Kiyovu 3-2 Bugesera Fc ( Uwanjani Mumena)
Espoir 0-0 Muhanga ( Uwanjani Kamarampaka
APR FC 0-1 Etincelles Fc (Uwanjani Kigali)
Amagaju 0-0 Gicumbi FC


Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments