LIVERPOOL YAISHANGAZA DUNIA

‘Majogoo wa jiji’ Liverpool wameushangaza ulimwengu kwa mara nyingine tena baada ya kutoka nyuma ya Borussia Dortmund na kufanikiwa kushinda mechi kwenye uwanja wa Anfield kisha kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa League.

Kikosi cha Jurgen Klopp walipigiliwa magoli mawili na kutakiwa kuhitaji kuifunga Doertmund magoli matatu ili kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Lakini vidume walipambana na kuupanda mlima huo kabla ya Dejan Lovren aliyetokea majeruhi kusukuma kambani krosi ya James Milner kambani na kuihakikishia ushindi timu yake.

Wakiadhimisha kumbukumbu ya miaka 27 ya janga la ‘Hillsborough’ ambapo takribani mashabiki 96 walifariki dunia kwenye dimba la Anfield, uwanja mzima ulisimama kutoa heshima kwa mashabiki hao kwa dakika moja kabla ya mechi kuanza ambayo itakumbukwa vizazi na vizazi vya mashabiki wa Liverpool.

Dortmund walipata magoli mawili baada ya dakika tisa za kwanza kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang na kuwa mbele kwa magoli 3-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Signal Iduna Park, Ujerumani juma lililopita.

Liverpool ilihitaji magoli matatu sasa ili kufuzu kwa hatua inayofuata, zikiwa zimesalia dakika 25 pambano kumalizika, Philippe Coutinho alipachika bao la pili kabla ya Mamadou Sakho kuongeza bao la tatu dakika ya 77 na kufufua matumaini ya uwezekano wa Liverpool kusonga mbele.

Alikuwa ni Lovren ambaye aliibua shangwe za mashabiki wa Liverpool dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kupiga bao lililoipa Liverpool ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Dortmund na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Europa League.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments