Ligi kuu ya Rwanda : APR FC, RAYON SPORTS warudi uwanjani

Baada ya wiki kamili ya kukumbuka mauji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, Mwishoni mwa wiki hii, Rayon sports itarejea uwanjani kwa kusaka ubingwa msumu huu.

Rayon Sports inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 nyuma ya APR Fc ikiwa na pointi 34 kwenye nafasi ya kwanza juu ya msimamo wa ligi.

APR Fc inahitaji ushindi ili kujitengeneza mazingira ya kutetea ubingwa wake, lakini italazmika kufanya kazi ziada kuifunga Etincelles kwenye uwanja wa Kigali.

Ijumaa

SC Kiyovu v s Bugesera FC
Espoir vs AS Muhanga
APR FC vs Etincelles
Amagaju FC vs Gicumbi FC


Juma pili

Police FC vs Mukura VS
Rwamagana City vs AS Kigali
Musanze FC vs Sunrise FC
Rayon Sports vs Marines FC

Mshambuliaji Hakizimana Muhadjili wa Mukura Vs bado anaongoza orodha ya wafungaji bora katika Azam Rwanda premier league na mabao tisa, Lomami andre wa Kiyovu Sports anashika nafasi ya pili na mabao 8.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments