Alitoa sarafu iliyotumika chini serikali ya Kayibanda kama zawadi ya kusaidia waliyenusurika.

Kijijni cha Birira, tarafa la Kimonyi, Wilayani Musanze, katika muda wa kukusanya misaada inayosaidia waliyenusurika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, Mtu bado hakujulikana alitoa sarafu iliyotumika zamani chini ya utawala wa Rais Kayibanda Gregoire juzi tarehe kumi mwezi Aprili.

Polisi na Ibuka wanasema kwamba hii ni ishara ya kukana mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Rwasibo Jean Pierre, Rais wa Ibuka wilayani Musanze alisema ‘’ishara hii ina lengo la kukana mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, inaonyesha kwamba Itikadi ya mauaji ya halaiki bado kumalizika.’’

Katika mahojiano na Izuba Rirashe aliongeza ‘’yeye alitoa sarafu ya pesa moja kipambwa kichwa cha Rais Kayibanda, tuliona kwamba ishara hii ina lengo la kukana mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi iliyotokea mwaka 1994.’’

Inspekta wa Polisi Gasasira Innocent, Msemaji wa Polisi mkoani kaskazini alithibitisha kwamba bado wanafuata mjinai huu.

Makala ya 135 katika kanuni za sheria nchini Rwanda inasema kwamba yeyote anakatwaa na hatia ya itikadi ya mauaji ya kimbari afungwa miaka tano hadi tisa pamoja na adhabu thamani elfu mia hadi milioni moja katika fedha la Rwanda.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments