KUKUMBUKA 22 : Upekee wa mauaji ya kimbari didhi ya watutsi.

1


Karne ya 20 iliachia dunia balaa nyingi kwani ndipo vita vya dunia vyote vilikuwepo na ukali wavyo ni wazi kueleweka, tukitazama undani mwa historia nzima mauaji ya kimbari didhi ya wayahudi, watutsi na mauaji ya kimbari nchini Cambodia na Bosinia katika karne hii ya 20.

Kiukweli mauaji ya kimbari yanafanywa kwa ukatili mkubwa kwani tunaona kuwa utu uligeuka unyama na watu wakaona kuwa mtu si mtu yaani ni mnyama na ni rahisi kumuua bila kujali mabadiliko yeyote baada ya kufanya maovu ya ukatili.

Mauaji ya kimbari didhi ya watutsi yana upekee maalumu ukilinganisha na mauaji ya kimbari yaliyokuwepo hapa duniani, hizi ndizo sababu zinazoonyesha kuwa mauaji haya ni tofauti kabisa wakati unapojalibu kulinganisha na mauaji ya kimbari mengine :

Watu zaidi milioni moja walipoteza maisha katika siku mia moja tu, inamaana kuwa watu mia moja waliuawa kwa kila siku.

Wanyarwanda walikua na mila na utamaduni sawa yaani lugha moja
Watu waliua majirani, watu kutoka ukoo mmoja, mme akaua mkewe na watoto hata na mamamkewe na babamkewe, watu walikuana na umoja na ushirikiano sawa punde si punde utu ukapoteka kama upepo.

utumiaji wa vifaa vya jadi visivyoua kwa uharaka kama mpanga, mkuki na vingine kwa lengo la kutesa wasio na hatia.

Wauaji walitumia ukatili wa ziada kama upakaji na kuambukiza UKIMWI , watoto kupigwa kwenye ukuta na kunywa damu ya wasio na hatia.

Ngazi zote za serikali zilishiriki katika mauaji ya kimbari kama madini.

Umaoja wa mataifa ulikuwa unaangalia mauaji bila kufanya chochote hata na usaidizi Fulani ili uokowe wasio na hatia.

Mauaji ya kimbari didhi ya watutsi yalisimamishwa na wanyarwanda pekee yao yaani wanajeshi wa RPF wakiongozwa na Rais Paul Kagame.

Katika mauaji ya kimbari didhi ya watutsi utu uligeuka unyama lakini tunaona mwanga kutoka mionzi na nguvu za wanyarwanda ambao wanashirikiana na kujenga taifa lao ili kuleta amani ya hudumu na maendeleo endelevu.

Katika habari hii tumetumia data ya CNLC, IKIGANIRO : KURWANYA GENOCIDE N’INGENGABITEKEREZO YAYO.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. katika Kizazi hiki vijana na Waschana ndio msingi wa kugombana na Vita vya Kimaneno ambavyo humdunisha na kumpuuza mtu Fulani ili kuonyesha ubaya wake usiokuwepo.
    Utekelezaji wa mauaji ya Kimbali nchini Rwanda ulisaidiwa na nguvu za Vijana walioitwa (Inerahamwe) ambao walijizoeza vita na kuwaua Raia watautsi.

Tumia Comments