NYANZA : Walikamatwa kwa kutuhumiwa kufanya sherehe ya ndoa katika wiki ya kukumbuka.

Mtu mwenye umri wa miaka 60 anaoishi katika tarafa ya Kibilizi wilayani Nyanza alikamatwa jana kwa kutuhumiwa kufanya sherehe ya ndoa katika wiki ya kukumbuka, kitendo hiki kinachukuliwa kama hatua ya kukana mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994.

Wakazi huyu alikamatwa pamoja na watu takriban kumi katika harusi ya mschana wake ambalo lilifanyika katika kijiji cha Mututu jumamosi iliyopita tarehe kumi mwezi Aprili 2016.

Katibu wa tarafa ya Kibilizi Bw. Jean Baptiste Habineza alithibitisha habari hii alisema kwamba watu wote waliohudhuria sherehe hii walikamatwa na polisi ka kutuhumiwa kukana mauji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Alisema ‘’mtu huyo pamoja na washiriki wote walikamatwa katika hatua ya kukana mauaji ya kimbari kwa sababu kufanya sherehe ya ndoa katika wiki ya kukumbuka ni hatua ya kukana mauaji ya kimbari.’’

Habineza aliongeza kwamba inajulikana nchini kote kufanya shuguli za burudani ni kinyume na sheria katika wiki hii.

Mkuu wa IBUKA wilayani Nyanza, Canisius Kayigamba pia alithibitisha kwamba watu hawa walikamatwa katika kitendo kinacho fanya maumivu walionusurika.

Katika mazungumzo na mwanahabari alisema’’nilijua habari hayo Mi namjua kamili ni msomi ,miaka mingi nyuma alikuwa mfanyakazi katika wilaya, labda alifanya hivyo kwa makusudi.’’

Watu waliokamatwa katika sherehe hii waleletwa katika kituo cha polisi inayofanya katika tarafa ya Muyira kwa kujibu kuhusu kitendo hicho kutokana na mujibu wa tarafa la Kibilizi.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments