Bado tunahitaji maelezo zaidi kuhusu watu wetu waliouawa katika Nyanza ya Kicukiro –Waziri Busingye

Waziri wa sheria na mjumbe mkuu wa Rwanda Johnstone Busingye anasema kwamba Rwanda na wanyarwanda kwa ujumla wanahitaji maelezo zaidi kuhusu watutsi waliouawa katika Nyanza ya Kicukiro wakati mauji ya kimbari dhidi ya watutsi yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Busingye amesema hilo wakati wafanyakazi wa wizara ya sheria (MINJUST) wakitembelea kituo cha kumbukumbu hapo Nyanza, Wilayani Kicukiro.

Busingye amesema’’bado tunahitaji majibu zaidi kuhusu watu wetu waliopoteza maisha hapa Nyanza ya Kicukiro.’’
Pia alisema kuwa yeyote aliyeacha waathirika badala ya kuwaokoa wakati alijua watauawa ahitajiwa kuulizwa zaidi kuhusu hilo.

Waziri Busingye aliomba pia viongozi katika ngazi zote kutotumia uwezo wao kutenda mambo kinyume na sheria kwa sababu haichangii chochote katika jamii husika.
Alikumbusha kwamba umoja wa Wanyarwanda ni silaha kubwa ya kupambana na ubaguzi wowote.

Zaidi ya waathirika elfu kumi na moja wazikwa katika kituo hiki ; waliawa baada ya kukataliwa na askari wa Umoja wa mataifa ambao walikuja kulinda amani nchini Rwanda.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments