Asili ya neno ’’Mauaji ya kimbari’’

1

Mauaji ya kimbari ni maangamizi ya mpango ya kundi zima la watu au ya sehemu yake kwa msingi wa utaifa, ukabila, rangi au dini.

Maneno "mauaji ya kimbari" yalianzishwa na Lemkin Raphael (mwanachuoni wa kisheria mwenye asili ya Kiyahudi aliyezaliwa nchini Poland 1900-1959), mnamo mwaka wa 1944, kwanza kutoka Kilatini "gens, gentis," kumaanisha "kuzaliwa, kabila, ukoo, aina" au mzizi wa Kigiriki "génos" (γένος) (maana sawa) ; pili kutoka Kilatini -"cidium" (kukata, na kuua) kupitia Kifaransa -"cide".

Lemkin alipoteza watu zaidi 50 katika mauaji ya kimbari didhi ya wayahudi kati mwaka 1939 na 1945.

Mwaka wa 1933, Lemkin aliitayarisha insha yenye kichwa : Uhalifu wa Kinyama ambapo mauaji ya kimbari yalionyeshwa kuwa uhalifu dhidi ya sheria za kimataifa. Dhana ya uhalifu, ambayo baadaye ilibadilika na kuwa wazo la mauaji ya kimbari, ilitokana na mang’amuzi ya Waashuri waliouawa kinyama nchini Iraq tarehe 11 Agosti 1933.

Wazo la Lemkin la mauaji ya kimbari kama kosa dhidi ya sheria za kimataifa lilikubalika na jamii ya kimataifa na lilikuwa mojawapo kati ya sheria msingi za Mashitaka ya Nuremberg (mashitaka ya viongozi 24 wa Kinazi) iliyotilia mkazo katika sehemu ya 3 kuwa watuhumiwa "walifanya mauaji ya kimbari kwa makusudi na kwa utaratibu - yaani, kuviaangamiza vikundi vya rangi na vya kitaifa.

Kiujumla, mauaji ya kimbari si lazima yamaanishe uangamizaji wa taifa mara moja, isipokuwa yanapofuatwa na mauaji ya halaiki ya watu wote wa taifa hilo. Inanuiwa kuashiria mpango wa hatua mbalimbali zenye nia ya kuangamiza misingi muhimu ya maisha ya vikundi vya kimataifa, zikiwa na nia ya kuviangamiza vikundi hivi vyenyewe.

Lengo la mpango kama huo utakuwa kubomoa miundo-msingi ya kisiasi na kijamii, ya tamaduni, lugha, hisia za kitaifa, dini na kuwepo kwa vikundi vya kitaifa kiuchumi, na uharibifu wa usalama wa kibinafsi, uhuru, afya, heshima na hata maisha ya watu binafsi katika vikundi hivyo.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. Kwa ufupi ! shukrani za dhati zimfikie mtangazaji huu kwa usaidizi usiokomaa wenze maelezo zaidi kuhusu asili ya neno"mauaji ya kimbari" endelea kutufahamisha mengi zaidi%

Tumia Comments