Tarehe ya Matembezi na Usiku wa kukumbuka imetangazwa.

Waziri Uwacu Julienne
Baada ya kuahirisha utembezi (walk to remember) na usiku wa kukumbuka, sasa waziri wa utamaduni na michezo Bi Julienne Uwacu tayari ametangaza tarehe ya matembezi na usiku wa kukumbuka itakafanywa.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, waziri huyu ametangaza kwamba baada ya kwambia wanyarwanda kuwa matembezi ya kukumbuka aliahirishwa kwa sababu ya mvua, Uwacu Julienne ametangaza kwamba Matembezi ya kukumbuka na usiku wa kukumbuka itafanywa tarehe ya tisa mwezi Aprili.

Julienne amekumbusha kila mtu ambaye atakayehudhuria hatua hii ya kukumbuka kwamba watakutana mbele ya ofisi la bunge saa nane mchana ambapo wataanzia matembezi ya kukumbuka kisha usiku wa kukumbuka utafanyika uwanjani wa taifa Amahoro.

Tangu jana Bendera la Rwanda linapepea nusu mringoti kwa kutoa heshima watutsi ambao waliuawa kinyama katika mauaji ya kimbari ambayo aliotokea mwaka wa 1994.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments