Rais wa Chad Idriss Deby awania muhula wa tano

Rais wa Chad ni miongoni mwa marais wa Afrika waliohudumu kwa mda mrefu madarakani anawania muhula wa tano wakati ambapo wapiga kura watashiriki katika uchaguzi mnamo tarehe 10 mwezi Aprili.

Rais Deby alitwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1990. Tangu wakati huo hadi sasa ameendelea kuthibiti taasisi muhimu za taifa na amekua mshirika wa karibu na dola za magharibi katika vita dhidi ya ugaidi.
Upinzani ulisusia uchaguzi mkuu wa mwaka 2011 na hivyo kumuwezesha kupata ushindi kwa urahisi.

Mwaka huu japo kuna upinzani lakini Bw Deby anatarajiwa kupata ushindi kutokana na mgawanyiko miongoni mwa wapinzani wake.
Aidha mahakama ya kikatiba imemzuia mpinzani wake mkuu kuwania pamoja na wagombea wengine watano.

Vyombo vya usalama vimevunja maandamano ya upinzani yanayomshinikiza Deby kuachia ngazi. Kinyang’anyiro cha urais nchini Chad kimevutia wagombea 13. Idriss Deby anapeperusha bendera ya chama tawala Patriotic Salvation Movement.

Wapinzani wake wawili ni mawaziri wake wa zamani. Ikiwa hakutakua na mshindi wa moja kwa moja ambaye anafaa kushinda asilimia 50 ya kura, basi itafanyika raundi ya pili ya kura ya urais kati ya mshindi wa kwanza na wa pili.
Chad imekabiliwa na changamoto za kiusalama tangu ijipatie uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1958.

Katika siku za karibuni nchi hiyo imekabiliwa na tishio la ugaidi kutokana na makundi yaliyo nchi jirani ya Boko Haram ya Nigeria na kundi la Al Qaeda tawi la Afrika Kaskazini linaloendesha operesheni zake katika mataifa ya Sahel.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments