Rapa AY ameunga mkono waathirika wa mauaji ya kimbari

Mwanamziki mkongwe katika ngoma za bonga flava (nchini Tanzania) anayejulikana katika nyimbo inatingisha bara la Afrika ‘’ZIGO Remix’’ pamoja na Diamond Platnum ameunga mkono waathirika wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ambwen Allen Yessayah AKA AY amewaombea (waathirika) kupumzika pema peponi.
‘’Nawaombea watu wa Rwanda amani na upendo, leo hii ni kumbukumbu ya mauaji ya kimbari miaka 22 iliopita…mzidi kujenga nchi kwa umoja…niko pamoja na nyi.’’
AY amesema.

Mwaka jana, Diamond (mtanzania), Tayo (kutoka Nigeria) Zari, mke wa Diamond na Chameleone AKA Sauti ya Dhahabu na Kadhaa ni miongoni mwa wasanii waliunga mkono wanyarwanda katika wiki ya maadhimisho.


Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments