Tukumbuke wasanii waliopoteza maisha yao katika mauwaji ya kimbari didhi ya watutsi.

Rugamba Cyprien ni baadhi ya wasani waliopoteza maisha yao.

Mwaka 1994,Rwanda ilipitia katika historia ya giza ambapo mauaji ya kimbali didhi ya watutsi alitokea, jamii ya wanyarwanda ilipoteza watu zaidi ya milioni moja.

Kuna wasani ambao walipoteza maisha yao katika mauwaji ya kimbali didhi ya watutsi ndio maana tumejaribu kuwaandalia orodha ya wasaii hao ambao tunakumbuka kwa mara ya 22.

Ingawa ni vigumu kuona orodha kamili ya wasanii hao kuna wasanii ambao tumejaribu kuona habari zao na tungependa kuwakumbushana wasani hao.

1.Rugamba Cyprien ni msani aliyetamba sana, jamii ya wanyarwanda haiwezi kumusahau kwani ndie alieanzisha kundi liitwalo Amasimbi n’amakombe na kujulikana katika nyimbo zinazojenga jamii ya wanyarwanda hata na nyimbo za injili nyingi zinazotumiwa katika dini la kikatuliki.

2. Sebanani Andre ni msanii amabaye alijulikana katika kundi la mzika iliitwalo Impala na kujulikana katika michezo ya kiigiza na kupitia kwenye redio Rwanda, hapa tungependa tutaje mchezo wa kuigiza uitwao icyanzo cy’Imana, Uwera hapo ndipo aliyecheza na kuitwa jina Kwibuka.

Sebanani Andre

3. Bizimana Roti msanii huyu alikuwa na upekee wake katika nyimbo zake na kupenda kukejeli sana, alijulikana katika wimbo kama Ntamunoza.

4. Karemera Rodrigue msani huyu hawawezi kusahaulika akilini mwa jamii kwani alikuwa mtaalumu pia alijifunza mziki, aadhi ya nyimbo alizoimba kuna HAGATI Y’IBITI BIBIRI na nyinginezo alizoimba katika lugha mbalimbali ikiwemo kifaransa, Kiswahili na kiingereza.

Karemera Rodrigue

5. Uwizeye john alitamba kwa wimbo wake uitwao AGASOZI KEZA KA RUSORORO.

Tunaweza kutaja wengine kama : Sekimonyo Emmanuel aliyejulikana kwa wimbo ”UMWANA W’UMUNYARYARWANDA” Niyigaba vicent , Gatete sadi wote walioimba kwenye kunda Abamararungu na Rugerinyange Eugene ambaye alimba katika kundi liitwalo Ingeri na Bizimungu Dieudone naye msani wa kipekee wote hawa walipoteza maisha katika mauwaji ya kimbali didhi ya watutsi mwaka.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments