Daraja la kimataifa la Rusumo limefungua rasmi

Rais Dkt John Magufuli leo hii ameanza ziara ya kikazi nchini Rwanda, siku hii Rais Kagame wa Rwanda na Rais Dkt John Pombe Magufuli wa Tanzania wamefungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha biashara chenye huduma muhimu wa kuunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kituo hicho kilichopo mpakani wa Tanzania na Rwanda kitasaidia shughuli za maendeleo za nchi husika na kuimarisha shuguli za maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki, na zile za ukanda wa bahari ya Hindi. Ni kituo kinachotumiwa na watu elfu mbili na magari145 abebayo mizigo kwa kila siku..

Baada ya shughuli hiyo, viongozi hao wataelekea mjini Kigali ambapo watakuwa na mazungumzo pamoja na kutembelea eneo la kumbukumbu ya mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi yaliyotokea mwaka 1994.

Ziara hiyo ya kwanza kwa Rais Dkt. Magufuli nje ya nchi, inaonyesha nia yake ya dhati kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuendeleza ushirikiano na nchi majirani.

Magufuli’’ Kagame ni rafiki yangu.’’

Kagame na Magufuli nchini Tanzania wamepokewa katika ngoma za jadi

Wakati wamerejea kufungua daraja la rusumo wamehudhuriwa katika heshima ya kijeshi

Wakazi wamehudhuria sherehe kwa idadi kubwa

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments