Tumukumbuke Daktari Martin Luther King

Daktari Martin Luther King Junior alikuwa ni Mchungaji wa Kibaptisti na Mwanaharakati mashuhuri kutoka nchi ya Marekani aliyepigania haki za binadamu.

Daktari Martin Luther alizaliwa tarehe 15 Januari 1929 mjini Atlanta, Georgia, Marekani. Alikuwa ni mtoto wa mzee Martin Luther king Sr na Alberta Williams King.

Alikuwa kiongozi wa kupigania haki za binadamu. Mnamo mwaka 1964 alitunukiwa tuzo ya Nobel ya Amani. Dr Martin Luther king alifariki dunia tarehe 4 Aprili 1968 kwa kupigwa risasi.

Alifunga ndoa na Coretta Scott King na kuzaa watoto wanne Yolanda Denise King, Martin Luther King III, Dexter Scott King, Bernice Albertine King. Moja ya mambo aliyofanya King ni kuongoza moja ya mgomo uliochukua muda mrefu katika historia ya migomo Marikani na duniani.

Aliongoza mgomo wa mabasi kupinga sheria ya kubagua abiria kutokana na rangi zao. Mgomo huu ulidumu kwa siku 382 hadi pale Mahakama Kuu ya Alabama ilitamka kuwa sheria hiyo ilikuwa inakiuka katiba ya nchi.

Mwaka 1963 aliongoza moja ya moja ya maandamano makubwa katika historia ya Marekani yaliyoitwa "March on Washington." Ni katika maandamano haya ndipo alipotoa hotuba yake maarufu ya "Nina Ndoto" (I have a Dream).

Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi alisema “nina ndoto kwamba siku moja taifa hili litasimama na kuishi kama inavyotamkwa kwenye imani yake. Nina ndoto kwamba siku moja watoto wangu wanne wataishi katika taifa ambalo hawatahukumiwa kutokana na rangi ya ngozi zao bali tabia/utu wao. Nina ndoto kwamba siku moja watoto wa waliokuwa watumwa na watoto wa waliokuwa wamiliki watumwa watakaa pamoja katika meza ya undugu.


Nina ndoto
Mwaka 1964 Dr. King alitunukiwa nishani ya amani ya Nobeli. Wakati wa kupokea tuzo hiyo alisema haya. Hotuba yake ya Nobeli nayo ina ujumbe mzito kuhusu mwanadamu na masahibu yake.

Dola 54,000 za Kimarekani alizopata kutokana na tuzo hii alizitumia kununulia vihamba (mashamba), magari ya kutanulia na kusafishia jina, na kujenga majumba ya kifahari ufukweni mwa bahari, !...We ! Nakutania. Aligawanya fedha hizo kwa vyama vilivyokuwa vikipigania haki na usawa. Unadhani Dr. King alikuwa kama viongozi wetu fulani na fulani ambao majina yao unayajua ?

Mwaka 1968 Dr. King aliuawa kwa risasi kama ilivyotokea kwa Malcolm X mwaka 1965. Au Mahatma Gandhi kule India. Au Lumumba. Au Che Guevara.

Alipigania haki ya binadamu

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments