Je,Mapenzi ya dhati ni kupigana picha za uchi ?

1

Mapenzi ni kitu kitamu sana katika maisha yetu ya kila siku, lakini hufurahisha mno wakati unapenda na wewe ukapendwa.

Siku hizi watu hupendelea kutumia aina mbalimbali kwa kuwasiliana na wapenzi, njia hizo hutokana na technolojia kama inavyoendelea kwa sasa. Vifaa vofauti kama whatsap, facebook, instagram na zingine, katika upande mwingine njia hizo hutumiwa kinyume kwa kufanya mambo yasiokubaliwa na jamii hata huiangamiza.

Kupigana picha za uchi imekuwa mila kwa siku hizi, na unakubali vipi kupigwa picha za namna hiyo. Wakati mwingine unaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa bila kupenda, kwa mfano simu au kamera yenye picha hizo ikipotea ujue hapo ni balaa, huwezi kuwa na amani hata kidogo.


Mapicha ya uchi kama haya yaweza kuwa na athari maishani mwako

Au aliyekupiga picha hizo mkigombana tu anaweza kukudhalilisha muda wowote. Chunga sana wengine hufikia hata uamuzi wa kujiua wakati akiona amepata aibu, na ujiona hana dhamani tena baada ya picha kusambaa.

Tuchukue mfano dhahili, ukipewa nafasi katika madaraka, kisha ikagundulika kuwa umefanya makosa ya kujipiga mapicha yanayoonyesha uchi wako, je unaona aibu hiyo kweli kama kiongozi !

Kweli tuchunguze na kufungua macho yetu baada ya kufanya jambo lolote kwani ni muhimu kutayalisha na kupanga mambo muhimu.

Martin Hubert IKURAMUTSE/ makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments