Majina ya ukoo/ familia katika lugha ya kiswahili

Haya ni majina ya heshima yanayotumiwa na watu mbalimbali katika familia
kulingana na uhusiano wao. Pia huitwa msamiati wa nasaba/jamaa/jamii

Familia Ndogo

Lengo letu ni kufundisha na kuendeleza lugha ya kiswahili kama kitambulisho cha jamii.

Hii ni familia ya karibu ambayo uhusisha tu wazazi na watoto wao.
1. baba : ( father )
ni mzazi wa kiume.
2. mama : ( mother )
mama ni mzazi wa kike.
3. mwana : ( child )
mtoto wako
4. mzazi : ( parent )
mtu aliyekuzaa
5. ndugu : ( sibling )
mtoto wa mzazi/wazazi wako. Mara nyingi ’ndugu’ hutumika kurejelea watoto waliozaliwa baada yako, au watoto wa kiume waliozaliwa na wazazi wako.
6. kaka : ( brother )
mvulana aliyezaliwa na mzazi/wazazi wako. Aghalabu kaka hurejelea mvulana aliyekutangulia kuzaliwa.
7. dada : ( sister )
msichana aliyezaliwa na mzazi/wazazi wako. Aghalabu dada hutumika kurejelea wasichana waliokutangulia kuzaliwa.
8. bin : ( son, mwana )
mtoto wa kiumeRais wa Marekani BARACK OBAMA

9. binti : ( daughter )
mtoto wa kike.
10. kifungua mimba : ( first born )
mtoto wa kwanza kuzaliwa
11. kitinda mimba : ( last born )
mtoto wa mwisho kuzaliwa
12. mapacha : ( twins )
watoto wawili waliozaliwa siku moja na mama mmoja
13. mke : ( bibi, wife )
mwanamke mliyefunga ndoa pamoja kuanzisha familia.
14. mume : ( husband )
mwanamume mliyefunga ndoa pamoja ili kuanzisha familia.
15. baba wa kambo  : ( stepfather )
mwanaume aliyeoa mamako, na ambaye si baba yako wa damu
16. mama wa kambo : ( stepmother )
mwanamke aliyeolewa na babako, na ambaye si mama yako wa damu

Katika habari nyingine tutaendelea na majina ya ukoo wa familia kubwa

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments