Waziri wa mambo ya nje wa Burundi atoa wito kwa wakimbizi kurudi nyumbani

Alain Nyamitwe waziri wa mambo ya nje wa Burundi akizungumza na VOA.
Katika mahojiano na VOA, Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw.Alain Nyamitwe amesema kwamba serikali yake imepokea vizuri suala la kuteuliwa rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa katika kusuluhisha mzozo wa Burundi.

Kuhusu wakimbizi walioko nje ya nchi hiyo ametoa wito wa wakimbizi hao kurudi na wasihofu usalama kwa sababu suala la usalama ni la wote wakimbizi na wale walioko nyumbani.

Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliteuliwa na jumuiya ya Afrika mashariki katika kutanzua mzozo wa Burundi hivi karibuni.

Maelfu ya warundi wakimbia katika nchi jirani na Burundi badaa Rais wa sasa Bw. Pierre Nkurunziza atangaza kushindana kwa muhula wa tatu katika urais.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments