UREMBO : Msamiati wa Mapambo


Mapambo ni vitu vinavyovaliwa na watu ili kujirembesha ; kuwafanya wavutie machoni pa watu wengine hivyo hivyo hupendelewa sana na wanawake isipokuwa kuna baadhi ya wanaume hupenda kuvalia mapambo hayo
.

1. Bangili : ( bracelet )
Ni pambo la duara linalovaliwa mkononi na wanawake.
2. Herini : ( kipuli )
Ni pambo linalovaliwa kwenye ndewe la sikio.
3. Hina :
Ni rangi nyekundunyekundu inayopakwa miguuni na mikononi mwa wanawake.
4. Kago : ( utanda )
Ushanga unaovaliwa kiunoni
5. Kanta :
Ni rangi nyeusi inayopakwa kwenye mvi (nywele nyeupe) ili nywele zionekana kama nyeusi, hasa na wale wasiopenda uzee.
6. Keekee :
Ni pambo linalovaliwa na wanawake mkononi kama kikuku au bangili.
7. Kigesi : ( anklet )
Nangili/kikuku kinachovaliwa na wanawake miguuni.
8. Kikuku :
Ni pambo la duara linalovaliwa mkononi au mguuni.
9. Kipini :
Pambo linalovaliwa puani (sehemu ya juu)
10. Kishaufu : ( hazama, kikero )
Hili ni pambo la duara linalovaliwa puani (sehemu ya chini).

11. Mafuta : ( oil, petroleum jelly )
Ni kitu kioevu kinachopakwa mwilini kwa makusudi ya kulainisha ngozi na kunukia vizuri.
12. Marashi : ( manukato )
Haya ni kifurushi, maji au mafuta yanayonukia vizuri yanayoundwa kwa mawaridi na kemikali nyingine yanayopakwa mwilini hasahasa kwapani.
13. Mkufu : ( necklace )
Ni kitu chembamba kama mnyororo kinachoundwa kwa madini kama dhahabu, fedha n.k kinachovaliwa shingoni.
14. Mshipi : ( belt )
Ni mkanda unaovaliwa kiunoni.
15. Ndewe :
Ni tundu linalotobolewa kwenye sehemu ya chini ya sikio ili kuvaliwa mapambo ya sikioni.
16. Ndonya :
Ni tundu linalotobolewa katika sikio na mdomo wa juu au mdomo wa chini
17. Nembo :
Ni chale zinazochanjwa usoni au kwenye sehemu nyingine za mwili. Nembo zilitumika kuonyesha kubaleghe(kuvunja ungo) kwa wasichana ; kubainisha kabila au kuonyesha urembo tu.
18. Njuga :
Kengele ndogondogo zinazovaliwa shingoni, miguuni na mikononi hasa wakati wa kucheza ngoma za kitamaduni.
19. Nti :
Ni vijiti vidogo vinavyovaliwa na wanawake masikioni baada ya kutoga ndewe.
20. Nyerere :
Ni uzi mwembamba wa madini unaovaliwa mikononi na miguuni.

21. Nywele bandia : ( wig )
Ni nywele za kununua zinazovaliwa na kina dada ili kujiongezea urembo.
22. Pete : ( ring )
Pambo la madini la duara linalovaliwa kidoleni.
23. Poda : ( powder )
Ni rangi nyeupe, laini itumiwayo na wanawake kujipaka.
24. Rangi ya kucha : ( nail polish )
Ni rangi inayopakwa kwenye kucha na wasichana
25. Rangi ya midomo : ( lipstick )
Ni rangi nyekundunyekundu inayopakwa kwenye midomo na wanawake.
26. Saa : ( hand watch )
Kifaa cha kupimia wakati kinachovaliwa mkononi kama pambo.
27. Tai : ( tie )
Nguo/kitambaa kilichoundwa ili kuvaliwa shingoni juu ya shati haswa wakati wa shughuli rasmi
28. Taji : ( crown )
Kofia inayovaliwa na wafalme, watawala au washindi kuashiria cheo chao au ushindi wao.
29. Ukaya : ( jebu )
Nguo au kitambaa kinachovaliwa kukinga sehemu ya mdomo hasa na wanawake Waislamu.
30. Usinga :
Nywele za farasi au nyumbu zinazovaliwa mkononi bangili.
31. Wanja :
Rangi nyeusi ya majimaji au ungaunga inayotumika na wanawake kupaka machoni, usoni, mikononi na hata miguuni.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments