Ladislas Ntaganzwa asafirishwa Rwanda

Ntaganzwa atajibu mashtaka nchini Rwanda.
Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, amesafirishwa kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kwenda nchini Rwanda ambapo atakabiliwa na mashtaka.

Kulingana na wakuu wa mashitaka nchini Rwanda,wanamtuhumu Ladislas Ntaganzwa kuongoza magenge ya wakereketwa wa kihutu waliofanya mashambulio dhidi ya watutsi,ugavi wa silaha na kuwabaka wanawake.

Kesi dhidi yake itasikilizwa nchini Rwanda baada ya mahakama ya kimataifa ya ICTR kufunga milango mwaka 2015. Kesi nyingine zitaendeshwa na taasisi iliyochukua nafasi ya mahakama hiyo.

Analaumiwa kwa kuongoza magenge ya wakereketwa wa kihutu waliofanya mashambulio dhidi ya watutsi,ugavi wa silaha na kuwabaka wanawake
Marekani ambayo ilitangaza zawadi ya dola milioni tano kwa mtu ambaye atasaidia akamatwe, ilimtaja kama moja wa wachochezi wakubwa wa mauaji hayo katika eneo la kusini la Butare.

Ladislas Ntaganzwa alikuwa amewekewa waranti wa kukamatwa na mahakama ya uhalifu nchini Rwanda ambayo ilimaliza shughuli zake mwezi Desemba mwaka 2015. Maelfu ya watu waliuawa nchini Rwanda mwaka 1994 wengi wao wakiwa ni watutsi.

Eneo la kuwakumbka waliouwa nchini Rwanda mwaka 1994.
Alikimbia Rwanda mwaka 1994 mara tu baada ya mauaji ya kimbari na kuchukua hifadhi katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Alikuwa kwenye orodha ya watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ambao bado wanasakwa kwa udi na uvumba dunia nzima na ambao serikali ya Marekani iliweka zawadi kwa yeyote atakayewakamata ama kutoa taarifa zitakazopelekea wao kukamatwa.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments