EU imefikia makubaliano kuhusu wahamiaji


Bi Merkel amesisitiza kwamba Ugiriki inahitaji usaidizi


Kwa mjibu wa BBC inasema kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya walioko kwenye mkutano nchini Brussels wameamua kwa pamoja kuwasilisha pendekezo moja kwa Uturuki, katika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi.

Katika mapendekezo ya mpango uliowekwa, wahamiaji wanaoingia Ugiriki kutoka Uturuki watarudishwa huku Uturuki ikipewa msaada wa kifedha na wakati huo huo raia wake kuweza kuingia barani ulaya bila visa.

Kansel awa Ujerumani Angela Merkel alilizungumzia baada ya mkutano huo wa umoja wa ulaya na Uturuki uliofanyika nchini Brussels.

Amesema Uturuki imekubali kukabiliana na umiminikaji wa wahamiaji kwa kupokea wakimbizi ambao wanarudishwa kutoka fukwe za Ugirikri ,fursa ambayo ni nzuri ili kwa kuwa inawaweka pembeni wafanya biashara haramu wa binadamu.

Hata hivyo suala hili linapaswa kuwa wazi kisheria, suala ambalo lilipewa mkazo zaidi katika mkutano huo.Tumekubaliana kuwa kila muhamiaji anayetoka katika fukwe ataweza kusikizwa yeye binafsi.

Ingawa chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel alisisitiza kuwa Ugiriki inahitaji msaada wakati ambao maelfu ya wakimbizi wamekwama nchini mwake.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kunahitajika makubaliano ambayo yataisaidia Ugiriki pamoja na Uturuki.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments