Tenisi : Wachezaji wahusishwa na kamari

Wachezaji wa tenisi waliohusishwa na kamari nchini Itali
Zaidi ya dazani mbili ya wachezaji tenisi wanafaa kuchunguzwa kuhusiana na uhusiano wao na michezo ya bahati nasibu,kulingana na mwendesha mashtaka nchini Itali.

Wachezaji hao wanashirikisha wachezaji wawili ambao wameorodheshwa miongoni mwa 20 bora duniani.

Kufikia sasa,ni wachezaji ,wataliano wawili ambao wamechunguzwa na kushtakiwa lakini Di Martino anasema wengine wanafaa kuchunguzwa.
Pia ameiambia BBC na Buzzfeed kwamba mamlaka ya tenisi inapaswa kujitahidi zaidi kutokana na ushahidi alioupata.

’’Kwa kweli iwapo wachezaji hawa wa kigeni ni Wataliano wanewkuwa wamehojiwa,alisema Di Martino.wangetoa maelezo’’.

Di Martino amekuwa akifanya uchunguzi wa miaka miwili kuhusu udanganyifu katika mechi unaowahusisha wachezaji wa tenisi na wachezaji kamari.

Uchunguzi wake umepata mazungumzo katika mitandao na rekodi za simu kati ya wachezaji na wachezaji kamari.

Chanzo : BBC

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments