Shabiki wa dortmund amepoteza afya uwanjani

Kwa mjibu wa azamu tv, gazeti hilo linasema kwamba kulikuwa na hali ya ukimya kwa muda wakati Borussia Dortmund ikipata ushindi wa bao 2-0 mbele ya Mainz kwenye ligi ya Bundesliga siku ya Jumapili.

Shabiki mmoja wa Dortmund alipata shambulio la moyo “heart attack” wakati wa kipindi cha kwanza katika mchezo huo na hatimaye akapoteza maisha.

Uwanja mzima uliokuwa na mashabiki zaidi ya 80,000 ulibaki kimya pamoja na mashabiki wa Mainz waliosafiri kwenda kwenye dimba la Signal Iduna Park kuishuhudia timu yako, wakifanya hivyo kwa kuheshimu kilichomkuta shabiki mwenzao wa soka.

Kwenye dakika ya mwisho ya kipindi cha pili, mashabiki wa Dortmund waliimba wimbo maarufu wa ‘You’ll Never Walk Alone’ ambao huimbwa na mashabiki wa Liverpool.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments