Katibu wa shirika la kandanda FERWAFA yumo mikononi mwa jeshi la polisi

Habari kufikia tovuti ya Makuruki.rw inaarifu kwamba katibu wa shirika la kandanda FERWAFA nchini Rwanda Mulindahabi Olivier, kwa sasa yumo mikononi mwa jeshi la polisi kwa ajili ya tuhuma za utoaji wa kibarua cha kujenga hoteli kwa njia iliyo kinyume cha sharia.

Kufuatana na habari ya msemaji wa jeshi la polisi nchini Rwanda ACP Celestin Twahirwa, amekanusha kwamba Bwana Mulindahabi yumo kabidhi mwa mwendesha-mashtaka kwa kukaguliwa na ngazi ya upelelezi kuhusu tuhuma anazozipachikwa. Maelezo juu ya matokeo ya upepelezi dhidi ya katibu huyu yatatangazwa baadaye mtuhumiwa kuhojiwa.

Jengo la hoteli ambalo lilitarajiwa kujazwa mahali karibu ya kikao cha shirika la kandanda FERWAFA, litachukua mchango wa kitita cha fedha biliyoni nne ambao utachangiwa na shirika la kandanda duniani FIFA. Hivi, Kibarua kilikwisha pewa kampuni ya Expert CEO LTD inayomilikiwa na mtajiri Protais Segatabazi pia aliyemo miongoni mwa wanaokaguliwa kuwa mhusika wa utapeli huo.

Kazi za ujenzi huu zilisimamishwa kukiwa na uvumi kwamba mshindi wa kibarua yumo upangoni na bado anakaguliwa kuhusu utapeli wa kupewa soko kwa njia isiyo halali.

Mmjoa baadhi ya mchambuzi wa suala hili amekiri kuna baadhi ya viongozi wa shirika la kandanda FERWAFA wanaotuhumiwa ila waliachwa huru kwa muda kwa sababu ya shindano la CHAN lilikuwa njiani kupamba moto nchini Rwanda.

Wakati bado kunaendelea ukaguzi, habari tofauti zinasema kwamba mtego huu huenda utafyatukana viongozi wengine katika shirika la kandanda baada ya shindano la CHAN kuelekea ukingoni.

Remy Niyingize

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments