Uganda : Jeshi la polisi la nunua silaha za ulinzi dhidi ya maandamano ya uchaguzi

Wakati nchini Uganda kunatarajiwa kufanyika uchaguzi wa rais, jeshi la polisi limejiandaa kukabiliana na waandamanaji dhidi ya vitendo vya uchaguzi ambapo imenunua silaha kali.

Ngazi ya uongozi wa la jeshi polisi nchini humu imethibitisha khabari hii kwa kutangaza kwamba silaha zilikwisha nunuliwa ni magari ya vita kwa mpango wa kuzuia maandano ya halaiki yanayoweza kuibuka wakati wa uchaguzi yakachafusha usalama.

Msemaji wa jeshi la polisi Fred Enanga akizungumza na vyombo vya khabari amesema kwamba wakati kwenye tarehe ya 18 mwezi, Februari kunasubiriwa uchaguzi wa rais, vifaa hivo vya kivita vilivyoandaliwa vitakuwepo ule wakati wowote upasao.

Amesema “ hatuna uhakika kwamba vurugu za maandamano zitatokea halafuye uchaguzi kujiri na hilo ikiwezekana kiukweli Waganda hawawezi kukubali litokee na hata hivo tuna uwezo wa kuzuia waandamanaji.”

Ijapo msemaji wa jeshi la polisi amekataa kutangaza idadi ya vifaa vinginevyo vya kivita vinapangwa kuongezwa , kiongozi huyu ametaja aina ya vifaa muhimu ambavyo vimekwisha wekwa tayari ikiwemo magari ya kulinda usalama, magari ya ujenzi ,magari ya kuzima ajali za moto, magari ya kupeleka wagonjwa hospitali na mengi mengineyo.

Msemaji Enanga ameongeza pia kwamba vifaa sio nchi tu bali vitachangia kwa mipango ya kulinda amani kwingineko kama ng’ambo ni ambapo nchi ya Uganda ilituma vikosi vya wanajeshi kwa ulinzi wa amani mathalani nchi za Liberia, jimbo la Darfur Sudani Kaskazini, Sudani Kusini na Somalia.

Remy Niyingize

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments