DR Congo mabingwa wa CHAN 2016


Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetwaa ubingwa wa kombe la Chan baada ya kuichapa Mali kwa mabao 3-0.

Magoli ya ushindi yalifungwa mchezaji Mechak Elia , aliwainua mashabiki mara mbili akifunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza , na bao la pili mapumziko huku mshambuliaji Jonathan Bolingi akifunga bao la tatu.

Huu ni ubingwa wa pili kwa timu ya taifa ya Dr Congo chini ya mwalimu Florent Ibenge kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Nayo timu ya taifa Ivory Coast imemaliza katika nafasi yaa tatu katika michuano hiyo baada ya kuichapa Guinea kwa Mabao 2-1.

DRC kwa mara ya kwanza , ilitwaa ubingwa mwaka 2009, mjini Abidjan
Tunisia ni mabingwa mwaka 2011 nchini Sudan

Libya ilitwaa ubingwa huo wa CHAN mwaka 2014 nchini Afrika ya kusini
Kwa mara ya 4 michuano hii iliyofanyika nchini Rwanda, DRC imenyakuwa taji la pili.

Mwaka 2018, CHAN itafanyika nchini Kenya.

Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Cote d’Ivoire baada ya kuizaba Guinea 2-1.

Mchezaji na mfungaji bora aliyechaguliwa ni mshambuliaji Mechak Elia.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments