EALA yapuuza tuhuma za Burundi dhidi ya Rwanda

Bunge ya umoja wa Afrika mashariki imetangaza kwamba inapuuza tuhuma za serikali ya Burundi dhidi ya Rwanda kuwa mchochezi wa kuzorotesha usalama nchini kwa sababu shahidi zilizopo hazina uhakika wowote kwa hivo haitazitilia maanani.

Ijumaa ya wikii hii kwenye tarehe ya 5 Februari, kamati ya katiba husika na migogoro na utatuwaji wa ugomvi katika kanda ya maziwa makuu imefanya mkutano wa saa sita kwa majadiliano ambapo imetoa ripoti yake katika bunge baada ya asilisho la kesi za umoja wa wanasheria wa Afrika PALU kuhusu haki za binadamu. Kamati hii imetoa uamuzi wake iliuchukua juu ya migogoro tofauti ilioikagua.

Baadhi ya migogoro iliyozungumziwa ilikuwemo kesi ya Rwanda kusaidia wapinzani wa serikali ya Burundi. Kesi hii ilipuuzwa kwa ajili ya tuhuma kutoka Serikali ya Burundi hazina shahidi zozote za kuaminika na licha ya hayo kufafanuliwa kwamba migogoro yoyote ya nchi ina ngazi nyinginezo za kisheria kuipitisha migogoro isipotatuliwa kwa ngazi fulani.

Kamati hii imebaini kuwa badala ya kukashfu nchi ya Rwanda kama mchochezi wa migogoro, lazima nchi mbili zikutane kwani inaonekana kuwa chanzo cha ugomvi nchini Burundi ni raia wenyewe kwa wenyewe.

Katika mkutano huu,kamati imependekeza kuwa upatanishi wa pande mbili ulioanza lazima urejelewe. Baadae Museveni Yoweli kuwa mpatanishi wa serikali na wapinzani wake , kamati imeomba upatanishi huo lazima utiliwe maanani tena , nguvu zaidi ziwekwe na idadi ya viongozi husika kwa upatanishi iongezeke ili migogoro nchini Burundi itatulike haraka ipasavyo.

Kuhusu suala la udhulumu wa haki za kibinadhamu wakati pande mbili pinzani zinatupiana makosa ya uhusika , kamati hii imependekeza kwamba dawa ni kuanzisha baraza la binafsi la kimataifa linalohusika na upelelezi wa migogoro ili washukiwa waadhibiwe kisheria.

Kwa upande mwingine, kesi ya kutuma kikosi cha kulinda Amani nchini Burundi,kamati imetangaza kuwa itatoa msimamo wake baada ya umoja wa nchi za Afrika kutimiza jukumu la kuanzisha baraza ilipendekeza pamoja na kuhakikisha likizuru nchi ya Burundi.

Remy Niyingize

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments