Bi Jeanette Kagame aeleza siri ya maendeleo ya Rwanda

Mke wa rais wa Rwanda Jeanette kagame katika sala ya kuombea amani nchi ya Marekani jijini Washington alifuchulia siri waliohudhuria sala hiyo siri ya maendeleo ya Rwanda.

Sala hii inayojiri kila mwaka, ilirejea jana ikiandaliwa na mkusanyiko wa Wamarekani na mashirika ya kikristo na ya kusambaza injili nchini humu.

Bi Jeanette Kagame alifunulia waumini siri kwamba hatua ya maendeleo ya nchi ya Rwanda inafuatilia mpango wa kuishi katika umoja kwa raia wote.

Alieleza kuwa nchi ya Rwanda ina tajriba kwa kuimarisha njia za kuishi katika umoja na usamehevu badae kupitia wakati mbaya za mauaji ya kinyama dhidi ya Watutsi yaliyojiri nchini mnamo 1994.

Aliongeza kuwa Wanyarwanda walishaanza safari ya kujithami, mradi ambao bado unahitaji mchango wa kila mtu na uongozi bora, hiari ya raia kwa kutumai viongozi wao bila ya kusahau upendo wa Mola kwani bila yake hakuna chochote kuwezekana.

Alisema “ Lengo tulilojipatia ni lile ambalo nchi ya Rwanda ilitia kipao mbele vitu vitatu muhimu ikiwemo umoja, kujipa majukumu kwa kila raia na kuwaza katika njia paana.”

Mwishoni Bi Jeanette Kagame aliwashauri waumini wa sala hii vitu viwili kama kusaidia wenzao kwa kuwasikia kwa dhumuni la kupata afya nzuri na kingine kuthamini maeneo wanapokaa.

Rais wa Marekani miongoni mwa waliohudhuria mkusanyiko huu alisisitiza kwamba kuwa na itikadi na tumaini ni dawa za uoga. Rais wa Marekani alipongeza mashirika ya wafadhili yanayochangia pakubwa kuangamiza mipango katili ya uuzaji wa wakimbizi badala yake wakawapokea.

Remy Niyingize

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments