Uwanja wa ndege aina ya Drones watarajiwa kujengwa nchini Rwanda

Inatarajiwa ifikapo katikati mwaka huu ndipo Rwanda itaanza kujenga uwanja wa ndege ndogo aina ya Drones.

Ndege hizo hazitakuwa na majukumu ya kupereka lisasi au Ujesusi kama aina ya ndege hizo zinavyofanya.

Majukumu ya ndege hizo yatakuwa ya kupereka dawa za matibabu maeneo ya vijijini ambako kuna usumbufu wa mabarabala.

Bwana Jonathan Ledgard kiongozi wa Afrika katika Tekinolojia akiongea na gazeti Swiss info, amesema kuwa Rwanda ilichaguliwa kama taifa la kwanza ambapo Serikari ya Rwanda ilikubali kuwapa maeneo ya kujenga uwanja huo wa ndege.

Sababu zingine zilizotajwa ni pamoja na kuwa Rwanda ina Rais Paul Kagame anae harakisha maendereo ya kiuchumi wa taifa kupitia ki tekinolojia.

Baada ya Rwanda kumalizika kwa ujenzi wa uwanja huo wa ndege Ethiopia ndilo taifa litakalo fuatia.

Tuwakumbushe kuwa uwanja huo unatarajiwa kujengwa katika Wilaya ya Bugesera Jimbo la Mashariki.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments