Matukio yaliyojili katika 1/4 Kombe la kimataifa CHAN

Katika michuwano ya kombe la kimataifa CHAN inayoendelea kuchezwa nchini rwanda kuna baadhi ya matukio yalioshangaza wapenzi wa soka.

Katika matukio hayo miongoni mwayo ni pamoja na timumu zote zilizokuwa zimefauru kuingia katika robo fainali zikiwa zakwanza katika kila kundi zilishindwa na timu zilizokuwa za pili katika kila kundi.

Timu iliyokuwa yakwanza katika kundi "A" Rwanda ilichapwa na timu ya DRC ambayo ilikuwa imefuzu kuingia robo fainali ikiwa ni ya pili katika kundi "B", Ambapo ilifanikiwa kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda.

Timu nyingine iliyoshindwa kuingia katika nusu fainali, ni timu ya Cameroun ambayo ilikuwa ikiongoza kundi "B" baada ya kuchalazwa na timu ya Ivory Cost ambayo ilikuwa imefuzu ikiwa ya pili katika kundi "A".

Timu ya Tunisia ilifanyiwa maajabu na timu ya Mali baada ya kuwa ya kwanza katika kundi "C" wakati timu ya Mali ilikuwa ni yapili katika kundi "D"

Wakati huo huo Timu ya Guinea ambayo ilikuwa imekuja kwa malayakwanza katika mashindano hayo ilifanikiwa kufuzu katika nusu fainali kwa kuishinda timu ya Zambia ambayo ilikuwa ni ya kwanza katika kundi "D" wakati timu ya Guinea ilikuwa ni yapili katika kundi "C"

Kwa machache ni hayo ambayo yanachukuliwa kama maajabu katika mashindano hayo yanayo endere nchini Rwanda katika kombe la kimataifa la CHAN.

Tuwakumbushe kuwa mechi za fainali zitachezwa hapo tarehe 7 Februari 2016 katika uwanja wa taifa Amahoro stadium.

John Bagabo

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments