Mfanyabiashara anasa pichaza mchumba’ke

DAR ES SALAAM : Mfanyabiashara wa bidhaa mchanganyiko (Machinga) aliyefahamika kwa jina la Khamis Kibiti amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunasa picha chafu za mchumba wake aitwaye Samia Sadiki akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Best Nassor katika pozi za kimahaba.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Khamis na Samia ni wachumba na wamekuwa na malengo ya kuoana hapo baadaye ila kuonekana kwa picha hizo kumemuweka njia panda Khamis.Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwa kudai kuwa picha hizo zilipigwa siku ya Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25, mwaka jana), kwenye moja ya nyumba ya kulala wageni jijini Dar.


Mfanyabiashara

Samia Sadiki akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Best Nassor.
“Hizo picha zitakuwa zilipigwa siku ya Krismasi mwaka jana maana siku hiyo Khamis alimtafuta sana mchumba wake kwenye simu hakupatikana kwa muda mrefu siku hiyo na hata kwao alipokwenda kumtafuta hakumkuta,” kilisema chanzo.
Kulingana na Risasi Mchanganyiko, :

“Nimekuwa nikisikia kwa muda mrefu kuhusu mchumba wangu katoka na msanii huyo ila sikuwa na vielelezo, nimejitahidi sana kuwavizia ikashindikana mpaka hivi karibuni niliponasa picha zao katika simu ya mchumba wangu.

“Nassor ameamua kumshawishi mchumba wangu na kutembea naye hivihivi, sitakubali nitakula naye sahani moja.”Baada ya kupata malalamiko hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mtuhumiwa (Samia) na kuzungumza naye.

Mchumba wa mfanyabiashara huro anayedaiwa kusaliti.

“Namfahamu Khamis kama mchumba wangu, Nassor ni kama shemeji yangu, ila kumekuwa na maneno yanayosemwa kuhusu mimi na Nassor ila ukweli sijawahi kutoka naye,” alisema Samia.

Gazeti hili lilimtafuta pia msanii huyo na kumsomea mashtaka yake ambapo alionekana kushangaa na kuhoji kuhusu upatikanaji wa picha hizo na kudai kuwa ni feki.“Duh ! Wewe umezipata wapi ? Naomba unitumie hizo picha, siyo kweli wamezitengeneza,” alisema Nassor.

Global publishers

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments