Al-Shabab : Kenya yanasa malori ya WFP


Serikali ya Kenya imeyanasa malori matatu ya shirika la chakula duniani WFP, ambayo inadai yamekuwa yakitumiwa kuwapelekea chakula wapiganaji wa kundi la al-Shabab.

Serikali ya Kenya imeyanasa malori matatu ya shirika la chakula duniani WFP, ambayo inadai yamekuwa yakitumiwa kuwapelekea chakula wapiganaji wa kundi la al-Shabab.

WFP imekanusha madai dhidi yake huku ikisema kuwa malori hayo yalikuwa yakipeleka shehena hiyo ya chakula hadi kambi ya Dholo Adow nchini Somalia.

Akizungumza na mwandishi wa BBC idhaa ya Kisomali Issa Ahmed, Afisa mkuu katika kaunti ya Mandera Fredrick Shisia amethibitisha kukamatwa kwa malori hayo matatu na amesema wanasubiri maelezo zaidi kutoka kwa maafisa wa shirika la WFP.

Ni ukweli tumekamata malori matatu yaliyokuwa yanaekejea Dholow Adow yakiwa na shehena ya chakula na bidhaa nyingine.

Hata hivyo nia yetu ya kuzuilia msafara huo ni kwa sababu tunahabari kuwa WFP inawaruhusu wapiganaji wa al-Shabab kuchukua chakula na bidhaa nyingine kutoka kwa mabohari yao nchini Somalia ambayo ni kinyume na makubaliano yetu nao.

’’Kenya haitaruhusu WFP iendelee kuwalisha maadui wa Kenya al-Shaabab kisha wakishiba wanarudi na kuishambulia Kenya na kudhuru raia wake,’’ alisema Bw Shisia.

shabab : Kenya yanasa malori ya WFP

’’Tunachotaka kwa sasa ni maelezo kamili kutoka kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP kujua kwa ni nani nayelengwa kupokea msaada huu wa chakula kabla ya kuruhusu msafara huu wa chakula kuingia Somalia," alisema Shisia.
Serikali ya Kenya ilinasa malori hayo katika kaunti ya Mandera Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Lori la nne la WFP lililokuwa limebeba magari liliruhusiwa kuendelea na safari.

Msemaji wa WFP, Bi Challis McDonough amethibitisha kuwa malori yao yamekamatwa nchini Kenya lakini anakana kuwa yalikuwa yanapeleka shehena hiyo ya chakula mikononi mwa wapiganaji wa al-Shabab.

Kumeibuka taharuki mjini Mandera kufuatia kukamatwa kwa malori hayo siku ya Jumamosi.


BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments