Rais Paul Kagame aungana na wanyarwanda kuwakumbuka mashujaa wa nchi

Tarehe Mosi Februari kila mwaka, Rwanda husherehekea siku kuu ya mashujaa wa nchi. Rais wa jamhuri Paul Kagame, akiambatana na viongozi mbali mbali wa serikali, maafisa wakuu wa kijeshi, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na wananchi kwa jumla wamesherehekea kwa mara ya 22 maadhimisho hayo.

Rais wa Jamhuri ya Rwanda Paul Kagame

Katika sherehe hizo, Rais Paul Kagame ameungana na wanyarwanda kusherehekea siku hii kutoa heshima kwa mashujaa.

Rais Kagame ameweka shada la maua kwenye makaburi ya mashujaa


Balozi anayawakilisha wenzake nchini Rwanda akitoa heshima kwa mashujaa wa Rwanda

Waziri wa michezo na utamaduni Julienne Uwacu, amesema kwamba Wanyarwanda wanatakiwa kuendelea kudumisha ushujaa wao kila mara, wametakiwa pia kutoa mchango kwa ujenzi wa taifa lao.

Waziri wa Michezo na Utamaduni Julienne Uwacu akiwa pamoja na Dr. Pierre Damien Habumuremyi, Kiongozi mkuu wa ngazi ya taifa inayohusika na mashujaa nchini.

Bi Uwacu ameongeza kuwa kuna mashujaa mbalimbali wakati huu, kulingana na vitendo mbalimbali vinavyofanywa. Amewataka wanyarwanda kutoa mchango wao kupambana na vita hiyo.

"Sote Wanyarwanda, tuna vita ya maendeleo. Kila mnyarwanda anapaswa kutoa mchango wake. Tunaposema hadhi yetu katika Rwanda ni kujitegemea’’, Waziri Uwacu Julienne amesema.

Julienne ameomba wanyarwanda kujihisi kama wanyarwanda wakiendelea kujenga umoja wao, na kupinga yeyote atakayewatenganisha akiwa nchini au nje.

Rwanda ina makundi matatu ya mashujaa ;

Kwenye kundi la mashujaa kuna Imanzi, ambako tunamkuta Maj. Gen. Fred Gisa Rwigema na hata askari asiyejulikani anayewasimamia askari wenzake waliokomboa nchi.

Katika kundi la Imena, kuna mashujaa wafuatao : Mfalme Mutara III Rudahigwa, Rwagasana Michel, Agathe Uwiringiyimana aliyekuwa Waziri mkuu wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, Felicité Niyitegeka na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Nyange.

Kaburi la shujaa Meja Jenerali Fred Rwigema

Katika kundi la Ingenzi hakuna watu waliotajwa

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema : "Duharanire Ubutwari, Twubaka Ejo hazaza." Ina maana kwamba Tuimarishe ushujaa, tukijenga taifa letu la kesho’’

Army Band wakitumbiza nyimboza kishujaa

Mwenyekiti wa baraza la Seneti Bernard Makuza na Mwenyekiti wa baraza la bunge Mukabalisa Donatille

Waziri mkuu Anastase Murekezi (upande wa kulia), Prof. Sam Rugege Mkuu mahakama kuu (upande wa kushoto) na Luteni Jenerali Karenzi Karake (upande wa nyuma) wamekuwa huko.

Rais Kagame akimusalimu Waziri mkuu Murekezi

Rais Kagame akimsalimu Hon. Bernard Makuza

Viongozi mbali mbali wakitoa heshima kwa mashujaa wa nchi

Rais Kagame akihitimisha sherehe za kuwakumbuka na kuwapa heshima mashujaa wa nchi.

Mahame Gilbert

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments