Rais Piere kushawishiwa

.
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.

Maafisa wamesema viongozi wa Afrika katika mkutano huo watajaribu kumshawishi Rais Piere Nkurunziza ambaye ndie aliechochea mzozo huo kutokana na kuwania muhula wa tatu madarakani katika uchaguzi wa mwezi wa Julai akubali kupelekwa kikosi hicho.Lakini pia wamesema hawadhani watafanikiwa kwa hilo.

"Linapokuja suala la vikosi, msimamo wetu haukubadilika ni mahala kusikoruhusiwa kupelekwa vikosi katika mazingira yoyote yale." Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Nyamwite amewaambia waandishi wa habari mjini Addis Ababa.

Kwa mujibu wa DW, Iwapo Umoja wa Afrika itapeleka kikosi hicho bila ya ridhaa ya Burundi itabidi itumie ibara ya nne ya katiba ya Umoja wa Afrika ambayo inaruhusu kuingilia kati katika nchi mwanachama iwapo hali ni mbaya sana kama vile : uhalifu wa kivita,mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litatakiwa litowe idhini ya mwisho.

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments