Suala Burundi kuhodhi agenda

Machafuko nchini Burundi.

Wakati mada rasmi katika mkutano wa AU ni suala la haki za binaadmu viongozi hao kwa mara nyingine tena wanakabiliwa na mkururo wa mizozo barani humo wakati wa mkutano wao wa siku mbili katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Mazungumzo katika Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yaliyohudhuriwa na marais na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama 54 wa umoja huo yaliendelea hadi wa usiku wa manane Ijumaa katika juhudi za kupunguza tafauti zao na kuwa na misimamo ya pamoja kabla ya kuanza rasmi kwa mkutano huo Jumamosi.

Mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma ameufunguwa mkutano huo wa kilele kwa kuwakumbuka walinda amani wa Umoja wa Afrika waliouwawa katika juhudi za kunyamazisha mapigano huku kukiwa na mdahalo mkali wa kupeleka kikosi kipya nchini Burundi.

Kulingana na DW, aadhi ya mataifa ya Afrika yanapinga kutumwa kwa kikosi hicho nchini Burundi bila ya ridhaa ya serikali ya nchi hiyo baada ya rais wa nchi hiyo kusema hatua hiyo itachukuliwa kama uvamizi wa nchi hiyo.

Hapo mwezi wa Disemba Baraza la Amani na Usalama la umoja huo lilitangaza mpango wa kupeleka kikosi cha wanajeshi 5,000 katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati ambapo mamia ya watu wameuwawa katika machafuko mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo tokea kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe chini ya misingi ya kikabila hapo mwaka 2005.

Suala la Burundi limepewa kipau mbele kikubwa katika agenda ya mkutano huo wa kilele wa siku mbili kutokana na ongezeko la matumizi ya nguvu kuitingisha kanda nzima ya Afrika ya Kati ambayo ina historia ya mizozo ya kikabila.

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments