Dr. Donald Kaberuka ateuliwa kuwa mjumbe wa fuko la amani AU

Dr. Donald Kaberuka apewa wadhfa wa kuwa mjumbe mkuu wa fuko la amani la umoja wa Afrika

Kiongozi mkuu wa tume ya umoja wa Afrika (AU), Dr. Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteua mnyarwanda Dr. Donald Kaberuka kuwa mjumbe wa fuko la amani la umoja wa Afrika.

Dr. Nkosazana, amesema kwamba hii ni ishara ya kuonyesha Umoja wa mataifa kwamba umoja wa Afrika AU una mwelekeo wa kujitafutia msaada wa kudumu kuhusu uungwaji mkono wa kurejesha amani chini ya uenyekiti wa Umoja Afrika.

Donald Kaberuka alizaliwa katika mkoa wa zamani wa Byumba mwaka 1951, alisomea chuo kikuu cha Dar es Salaam , masters alisomea chuo kikuu cha Anglia mwaka 1979, baadae alisomea uchumi kwenye chuo kikuu cha Glasgow na kupata stashahada ya PHD.

Kuanzia mwaka 1997, Kaberuka alikuwa waziri wa mipango na fedha nchini Rwanda , alifanikisha kuinua sekta ya uchumi wa nchi ambayo ilikuwa imekumbwa na mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi 1994.

Kuanzia julai 2005, Kaberuka alichaguliwa kuongoza benki ya maendeleo barani Afrika BAD, lakini alianza rasmi kazi hiyo mwezi oktoba mwaka huo, alifanya kazi kwa mihula miwili hadi mwaka 2015.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments